SAFARI YA KIIMANI, HUDUMA ZA KANISA

Karibu
KKKT Digital
Karibu KKKT Digital
Kituo cha Kuungana Kidijitali

KKKT Digital ni mfumo rasmi wa Kanisa unaotumia SMS, WhatsApp, na barua pepe ili kuimarisha ushirikiano na kuwapa waumini taarifa kuhusu mahubiri, maelezo ya matukio, na mafunzo kuhusu ujuzi wa maisha, ujasiriamali, na maendeleo ya imani.

Jinsi KKKT Digital Inakusaidia

KKKT Digital ni mfumo rasmi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) unaolenga kuimarisha ushirika kati ya Kanisa na waumini wake kwa njia ya teknolojia. Kupitia mfumo huu, kila msharika anaweza kupata taarifa muhimu za Kanisa popote alipo kupitia SMS, WhatsApp, Barua Pepe, na majukwaa mengine ya kidijitali.

Kupitia KKKT Digital, waumini hupokea muhtasari wa mahubiri, taarifa za matukio, elimu ya stadi za maisha, na mafunzo mengine kama ujasiriamali, teknolojia, malezi ya vijana, na mambo mengine yanayolenga kukuza huduma na imani ya kikristo.

Viwango vya Uchangiaji kwa Washiriki

Ili kufanya mfumo huu kuwa endelevu unaombwa kuchangia kiasi cha fedha kutegemeana na kifurushi(package) utakayochagua.

Shaba

Kwa msukumo wa msingi na ukuaji wa kiroho.

TSh. 36,000
KWA MWAKA MMOJA
Anza Kujisajili Sasa Malipo ya simu na benki yanapatikana
Vipengele Muhimu:
Mahubiri na Tafakari ya neno
Taarifa kuhusu kanisa, dayosisi na usharika wako
Maono, Malengo na Mipango ya Kazi
Mahusiano na Maadili ya kijana mkristo
Ukuaji wa kiroho na maadili ya Kristo
Maarufu

Fedha

Kwa mwongozo wa kina katika imani, maisha, na uongozi.

TSh. 50,000
KWA MWAKA MMOJA
Anza Kujisajili Sasa Malipo ya simu na benki yanapatikana
Kila kitu katika Shaba, pamoja na:
Ujasiriamali na fedha
Uongozi na huduma
Maono, Malengo na Mipango ya Kazi
Mahusiano na Maadili ya kijana mkristo
Ukuaji wa kiroho na maadili ya Kristo

Dhahabu

Kwa ukuaji kamili wa imani, ujuzi, na fursa za kisasa.

TSh. 80,000
KWA MWAKA MMOJA
Anza Kujisajili Sasa Malipo ya simu na benki yanapatikana
Kila kitu katika Fedha, pamoja na:
Elimu ya afya ya kimwili na kiakili
Teknolojia, AI na fursa
Ujuzi kidijitali na Mtandaoni
Maono, Malengo na Mipango ya Kazi
Uongozi na huduma

"KKKT Digital imebadilisha jinsi ninavyowahudumia washarika. Ilikuwa changamoto kufikisha ujumbe kwa haraka, lakini sasa waumini wanahusishwa zaidi na wanafikiwa mara moja. Mfumo huu ni daraja la mawasiliano kati ya Mchungaji na Usharika."

Mchungaji

Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara

  • Je, taarifa zangu binafsi kwenye KKKT Digital zina salama?

    Ndiyo. KKKT Digital inatumia viwango vya kimataifa vya encryption na sera madhubuti za faragha ili kulinda taarifa zako binafsi.

  • Je, kuna malipo yoyote ya kutumia KKKT Digital?

    KKKT Digital inatoa huduma kulingana na vipengele mbalimbali. Kila kipengele kina thamani tofauti kulingana na huduma zinazopatikana kama vile idadi ya jumbe zinazosambazwa, elimu mbalimbali za kimaisha kama ujasiriamali, teknolojia na mengineyo.

  • Ni kwa namna gani mfumo huu unawezesha mawasiliano ndani ya kanisa?

    KKKT Digital inawezesha mawasiliano kwa kufikia wanachama kwa wengi kwa wakati mmoja na kwa urahisi kupitia njia za mawasiliano kama SMS, WhatsApp, na Barua pepe. Hii inahakikisha wanachama wanapata taarifa muhimu haraka na kwa urahisi, huku kanisa likiimarisha uhusiano na mshikamano wa kijumuiya.

  • Nani anastahili kujiunga na kutumia mfumo huu?

    KKKT Digital imeundwa kwa ajili ya waumini wote wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT). Jukwaa hili linahusisha waumini wa dayosisi zote likiwa daraja la kuwezesha mawasiliano kidijitali ndani ya kanisa la kilutheri Tanzania.

  • Je, ni hatua gani mahususi zitakazochukuliwa ili kuhakikisha kwamba ujumbe unawafikia walengwa husika?

    KKKT Digital itahakikisha ujumbe sahihi unawafikia walengwa kwa kutumia uchambuzi wa taarifa na kugawa kwa makundi kulingana na umri, parokia, au maslahi ya kiroho. Mfumo pia unarahisisha urekebishaji wa ujumbe ili kufikia makundi maalum kama vijana, wazee au familia. Hivyo, kila muumini anapata taarifa, maombi, taarifa za matukio na mahubiri yanayomhusisha moja kwa moja.

Wasiliana Nasi

Tafadhali wasiliana nasi kwa kutumia njia zilizo hapa chini, na timu yetu itajibu maswali yako haraka iwezekanavyo.

Una swali au maoni? Tafadhali jaza fomu hapa chini, na tutaribu kurudisha majibu haraka iwezekanavyo.

Au tuma ujumbe kupitia info@kkktdigital.co.tz au +255 716 354 937 .